AINA MBILI ZA WAAMINI na Mwl. Dr Mwakisisile
Aina mbili za waamini (Two kinds of believers): Aina ya kwanza ni Christ conscience (dhamiri zao zinamtanguliza Yesu ) na ya pili ni devil conscience (dhamiri zao zinamtanguliza shetani ). Aina ya kwanza ni hali ambayo mtu katika mambo yake anaamini Yesu yupo naye. Akiamka asubuhi anamtukuza Yesu kwa kuwa naye usiku, akitoka nyumbani anaamini malaika anamtangulia katika njia zake zote. Hana haja ya kupambana na shetani. Mtu huyo haishi kwa hatari bali kwa amani na ujasiri. Likitokea tatizo anaamini uaminifu wa Mungu umemzunguka na ataibuka mshindi. Hampi sifa shetani katika mambo yake yote, anaamini kazi ya Yesu kuliko shetani. Huamini siku zote kuwa Mungu mwaminifu yuko naye popote. Kinywani mwake anamtaja Yesu na shetani hana nafasi. Hawezi kupoteza muda kuzungumza kazi za shetani maana kazi aliyofanya Yesu ni bora kuliko shetani. Akirudi usiku kulala anamshukuru Mungu kwa uaminifu anaamini Malaika wapo naye kumlinda, halali kwa hofu ya shetani maana anajua hakuna namna shetani atamfikia. Katika maombi na shuhuda zake, umtukuza Mungu na shetani hana nafasi. Aina ya pili ni waamini ambao wanaamini sana maneno ya biblia yanayomtaja shetani kuliko uweza wa Mungu. Akiamka asubuhi akili umwambia shetani yupo mlangoni, njiani au sehemu ya kazi. Uanza siku kwa kupambana na shetani, anaamini shetani anaongozana naye njiani bila kuamini malaika. Likitokea jambo baya atasema shetani amesababisha , Likitokea zuri atasema shetani ameshindwa. Mahubiri na maombi yake yamejaa shetani na kazi zake. Haamini juu ya uweza Mungu bali shetani. Akienda kulala humwona shetani akipenya ukutani kumfikia. Sehemu kubwa ya waamini hutumbukia kwenye kundi hili. Ukiwa katika kundi la kwanza kundi hili ambao ni wengi watakuinukia na kukuona msaliti. Hawataki kusikia habari ya uweza wa Mungu, watakwambia habari za watu waliopata mabaya kama ushahidi ya uweza wa shetani. Je wewe mpendwa upo kundi gani? Amina
No comments: