ULIMI na Mwl.B.Mwaijumba
UNAUTUMIAJE ULIMI WAKO EWE MKRISTO?(KINYWA CHAKO)
Mithali : Mlango 18:21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi;Na wao waupendao watakula matunda yake
.
Neno la Mungu limeweka wazi kuwa mauti na uzima upo katika ulimi wako . Watu wengi wamrjiangamiza kwa kutokujua kuutumia ulimi wao Yale unayo yatamka katika KINYWA chako ndio yanayo jenga uzima wako au kubomoa.
1wakoritho 15:33 Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.
Maneno unayo ongea yanajenga tabia njema au kuwa mbaya
Mithali :12:14 Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake;Na atarudishiwa matendo ya mikono yake.
Mithali 13:2 Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake;Bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri.
Mithali 18;20 Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake;Atashiba mazao ya midomo yake.
Mafanikio yako kushindwa kwako kunategemeana na Yale unayo tamka. Mungu ametupa KINYWA na akili ili tukitumie katika manufaa.
Mithali 6:2 Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako,Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,
Umeshindwa kusonga mbele kwa sababu umejirogo mwenyewe kwa maneno ya KINYWA chako Neno la Mungu lina ahadi nyingi zenye mafaniko lakini watu kwa kukosa maarifa waacha kuzikiri na kuzitwaa kuwa zao na wanabaki na matatizo yao na kushindwa wameshindwa kuutumia uwezo uliopo katika KINYWA chao tumia KINYWA chako vyema ili upate matunda kwa KINYWA chako
*************
Ulimi ni kiungo kidogo chenye madhara makubwa
Yakobo3:5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
Ulimi umevunja ndoa za watu umeondoa amani katika jamii, vita vingi vinatoke sababu ya ulimi .mpendwa unautumiaje ulimi/KINYWA chako neno la Mungu limetuagiza KINYWA chetu kijae maneno yaliyo kolea munyu
Wakolosai : 4:6 Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
Inasikitisha kanisa limegeuka uwanja wa kurushiana maneno kusemana mtumishi huyu anamsema huyu tena katika madhabahu. Watu wengi wameshindwa kumfuta kristo baada kuona maneno yanayo semwa na watu walio okoka na wanao sema Yesu ni Bwana. Tumia ulimi vizuri ulimi ni chemichemi ya uzima.

No comments: