Header Ads

test

HUKUMU INAKUJA na Mwl.Nathanael Chaligha

!!!!!!!! HUKUMU INAKUJA !!!!!!!!!!!!
          Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa,na mmoja aliye MZEE WA SIKU ameketi.
Mavazi yake meupe kama theluji.
na nywele zake kama sufu safi.
KITI CHAKE CHA ENZI KILIKUWA MIALI YA MOTO,
NA GURUDUMU ZAKE MOTO UWAKAO
   MTO KAMA WA MOTO UKAPITA  MBELE ZAKE,
Maelfu elfu wakiamua,
na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake.
HUKUMU IKAWEKWA,NA VITABU VIKAFUNULIWA. Daniel 7:9-10
      Yapo MATUKIO makubwa matatu hivi,yaliyoko mbele yetu ambayo hayana budi kuwako. 1:-KURUDI KWA YESU MARA YA PILI KULINYAKUA KANISA
                          2:-VITA KUU YA MWISHO(HAR-MAGEDONIA)NA KUFUFULIWA KWA WAFU
                            3:-HUKUMU YA MWISHO NA KWENDA UZIMA WA MILELE(YERUSALEM MPYA)AU MOTO WA MILELE(JEHANUM)
         HUKUMU YA MWISHO:-
      Hukumu inakuja mbele yetu mpendwa. Napenda ndugu yangu kukumbusha kuwa siku inakuja nayo iko karibu,utakayosimama mbele za Mungu kutoa hesabu ya maisha yako yote uliyoishi hapa duniani.Warumi14:12.
Mbona basi wamhukumu ndugu yako??
Au wewe je, Mbona wamdharau ndugu yako??Hivi hujui kuwa SISI SOTE TUTASIMAMA MBELE YA KITI CHA HUKUMU CHA MUNGU??Warumi14:10.
Hii ni pamoja nawe unayesoma makala hii. Paulo anaposema ," SISI SOTE" Ina maana ni pamoja na yeye.Na kama mtume mkuu wa Mataifa atasimama kupokea ijara yake ya mambo aliyotenda katika mwili,Je mimi na wewe tutaponea wapi??? HAKIKA SISI SOTE TUTASIMAMA MBELE YA KITI CHA HUKUMU CHA MUNGU.
  Kwa maana IMETUPASA SISI SOTE kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo,ili kila mtu apokee ijara(uzima au mauti)ya mambo ALIYOTENDA KWA MWILI,kadri alivyotenda,kwamba ni mema au mabaya. 2 Wakorintho 5:10
Kitakachotazamwa ni mambo yale ULIYOTENDA KWA MWILI WAKO.
Fikiri vizuri mpendwa ,kwani matendo yako yote na maneno yako yote,na mawazo ya moyo wako ,yote yametunzwa na kuwekwa kwenye vitabu vya Mungu,ili kuwa kumbukumbu Kwa siku ya hukumu.Ufunuo 20:11-15; Mathayo12:36;Warumi2;16
Siku Ile siri zote za wanadamu zitakuwa peupe,na kila mtu ataona,kwani itakuwa mahakama ya wazi na kila mmoja wetu atakuwa pale,tangu Adamu mpaka mtu wa mwisho,wakati ya parapanda ya mwisho.
Maneno yote uliyonena yamehifadhiwa ili siku ya hukumu uyatolee hesabu  Umenena mangapi ndugu?? Una hakika,yote uliyonena hayana walakini??
Watafiti (researchers)wanasema,mwanadamu kwa wastani ananena maneno 352 Kwa wiki,ambayo yakikusanywa pamoja yanaweza yakatengeneza vitabu 3000 kwa Mwaka.Je, mpendwa katika vitabu vyote hivyo,na maneno yote hayo umsafi??? Mimi sijui una uangalifu kiasi gani na yale uyanenayo kwa kinywa chako. Wajibu wangu ni kukueleza tu kuwa,"Kweli nuru ni tamu,tena ni jambo la kupendeza macho kutazama jua,Naam mtu akiishi miaka mingi,na aifurahie yote,lakini azikumbuke siku zijazo za giza(jehanum)kwa maana zitakuwa nyingi.(milele)
Wewe kijana,uufurahie ujana wako
na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako,(anasa na starehe)
Ukaziendee njia za moyo wako
na katika maono ya macho yako.
Lakini ujue wewe ya kwamba Kwa ajili ya hao yote
MUNGU ATAKULETA HUKUMUNI. Mhubiri11:7-9
   Unajiandaaje,rafiki na hukumu hii inayokuja?? Inatisha siyo???Wewe unaonaje,kusimama mbele ya Hakimu aliye na mambo yako yote?? Ambaye hahitaji shahidi wa mambo yako.Anayajua yote A to Z. Yohana2:24-25 .Siku ile itakuwa ngumu sana kwa wanafiki. Nadhani mbele ya kiti cha hukumu watapata shida kuliko wengine wote. Walijitahidi,huku duniani kuficha madhambi yao,na kujifanya wema Kwa nje,kumbe siyo. Wakasali sala ndefu na kujionyesha kwa watu kuwa wao ni watakatifu wa daraja la juu kabisa,kumbe siyo. Kwa siri wanakula kwenye nyumba za wajane(wazinzi).Ni waongo,wazushi,ni watu wa tamaa za kidunia tu,kama wanadamu wengine.Wanajificha katikati ya waliokoka,na kufanya Matendo yote ya waliokoka(Matendo ya nje tu)wanasalimu "BWANA YESU ASIFIWE" kama waliokoka,wanahubiri ,kuombea wagonjwa na kukemea pepo kama waliokoka,wanakiri kuwa wamezaliwa mara ya pili(born again) ,lakini ukweli siyo. Ni waongo tu na wanafiki ,Yesu alisema,mtawajua Kwa matunda yao. Nasema,hawa watapata shida sana.Mafarisayo wale na mafarisayo wa kizazi chetu,itawawia ngumu sana siku Ile. Hukumu itawaumbua. ITAKUWA AIBU KUU.
Hebu fikiri kidogo, Huku duniani ulikuwa kiongozi wa kiroho,wa watu 500;000; hivi.
Machoni pao ulikuwa mtu mwema,Mtakatifu na mwenye bidii nyingi,na wakikutukuza na kushuhudiana kuwa mbinguni ni kwako,na wewe ukijua hivyo,na kumbe Kwa siri unayo mambo ambayo wao hawajui. Siku Ile uchafu wako wote unawekwa wazi,mbele ya wale uliowaingoza. Na neno gumu kuliko yote uliyowahi kusikia maishani mwako,linatamkwa masikoni mwako ,"ONDOKA KWANGU ULIYELAANIWA,NENDA KATIKA MOTO WA MILELE" Mathayo25:41
Ni aibu siyo??? Mbele ya waumini wako?? Kwanini Mungu asikustahi wewe mtumishi wake??? Utaanza kujitetea, "Bwana umesahau,nilitoa unabii Kwa Jina lako,Kwa Jina lako nilitoa pepo,na Kwa Jina lako nilifanya muujiza. Pamoja na majiteteo yote hayo,Hakimu,MHUKUMU wa Haki anazidi kukaza hukumu,"ONDOKA KWANGU SIKUJUI KAMWE" Mathayo7:21-23
   Mmh!!! Hakujui kamwe?? Na utumishi wote ule!!!!!!
       Ewe,mnafiki,na mdhambi, jioshe sasa,tengeneza maisha yako ya sirini. Mungu anakuona.Yesu Kwa sasa ni mwokozi wako,amekaa kwenye "KITI CHA REHEMA" Bado kitambo kidogo sana,hatakuwa mwokozi tena,bali HAKIMU,akiwa amekaa kwenye,"KITI CHA HUKUMU"
Jinyenyekeze kwake,usafishe moyo wako sasa,kwani muda wa kufanya hivyo umefikia mwisho. Karibu mlango wa toba kufungwa.Angalia usichelewe.

Napumzika, nikirudi nitagusia hukumu ya wamwaminio Kristo,na mengine mengi.

No comments:

Powered by Blogger.