HISTORIA YA KANISA NA Mwl. N Chaligha
HISTORIA
YA KANISA NA UKRISTO WETU!!!
Hapo mwanzo wanafunzi wa Yesu
hawakujulikana kwa Jina la "WAKRISTO"
Kwa mara ya kwanza
waliitwa,"WAKRISTO" huko Antiokia. Matendo 11:26
Baada ya Bwana Yesu
kufa,kufufuka na kupaa,wanafunzi walienda huko na huko(ulimwenguni kote )
kuhubiri injili.
Baada ya mafanikio ya
mwanzo ya Injili yaliyopelekea maelfu ya watu kuongoka,wanafunzi walifanya kosa
la kuanzisha Kijiji cha ujamaa. Badala ya kulipeleka jeshi kwenye kazi ya
injili.,walifanya kazi ya kumega mkate nyumba kwa nyumba. Matendo2:44-47
Hii ilipelekea jeshi la
adui,kuingia ndani ya kanisa na kuleta choyo,ubinafsi,ulafi ,magomvi na
manung'uniko. Matendo 6:1
Kanisa la Mungu,mahali
popote na wakati wowote linapoacha huduma ya Injili kwa wadhambi na kubaki
kujitazama lenyewe(tule nini,tunywe nini,tuanzishe miradi gani,tujiimarisheje
kifedha)basi Kanisa hilo litegemee magomvi yasiyoisha Kati yao. Hata mbwa
asiyefundishwa kuwinda huwa mwizi wa mayai.
Ili litimie kusudi la
Mungu la kuhubiri injili kwa kila kiumbe,Mungu alikivunja Kijiji chao Kwa
kuruhusu mateso kwao baada ya kifo cha Stefano.Tunasoma kuwa Sauli(Paulo
)akaliharibu kanisa,akiingia nyumba kwa nyumba na kuwaburuta wanaume na wanawake
na kuwatia gerezani.Matendo8:1-3
Hii ilisaidia sana kuenea
kwa injili,kwani iliwapelekea watu wote kutawanyika na kwenda huko na huko
wakihubiri neno.Matendo8:4
Ndipo Mungu akaongeza
nguvu kwenye jeshi la Bwana kwa kumwongoa Sauli(Paulo )
Ashukuriwe, Mungu kwani
mtu huyu Kwa ujasiri wake UKRISTO ulienea kwa kasi kwenye nchi za
kipagani(Rumi,n.k.)
HISTORIA
YA KANISA NA UKRISTO WETU (2)
Katika maelezo yangu ya kwanza,nilieleza
kidogo kuwa Mungu alimwingiza Paulo katika huduma ya Injili.
Mitume walienda huko
na huko hadi Asia ndogo,India, Ethiopia
hadi Afrika Kaskazini.Petro na Paulo walihubiri huko Rumi(Italia)
UKRISTO HUKO RUMI:
Wakristo wa Kanisa la Karne ya 1-3
walipata mateso makali sana. Waliteswa sana na wapagani wa wakati huo.Na haya
mateso hapo Rumi yalikuwa makali sana.Mtawala mmoja aitwaye Nero alijulikana
kwa ukatili wake. Ndiye aliyemwua Petro.Wakristo walitupwa katikati ya simba
wengi wenye njaa ili waliwe. Wengine walitupwa kwenye matanuru ya moto wakiwa
hai.Wengine walisulubishwa(Petro) na wengine waliuwawa kwa kukatwa
vichwa(Paulo)
Kuwa Mkristo na kuhubiri
Kwa wakati ule kulimaanisha mateso na kifo.
Njia ya Yesu ni njia ya
dhiki na mateso tangu mwanzo wake hadi mwisho wake.Matendo14:22 .Mimi naamini
kipimo cha Mkristo mwaminifu ,ni dhiki udhia,mateso,vifungo,kukataliwa,kutengwa
na masinagogi. Vizazi vyote,na hata sasa watu waaminifu wamelipia gharama ya
ukristo wao(mateso).Hata mwandishi wa makala hii amewahi kulipia gharama
hii.Amefungwa gerezani Mwaka mmoja kwa ajili ya Yesu(1978) Amewahi kufukuzwa mara
3 akihubiri injili. Mara moja alifukuzwa Kwa mawe.Mwaka 1992 alipona kupigwa
risasi huko Mbozi(Mbeya)wakati akihubiri Injili,ikamlazimu kutembea usiku kucha
bila viatu kwenye barabara ya kokoto. Amewahi kutengwa na sinagogi,na kunenwa
vibaya mara nyingi kwa ajili ya Injili.
Najua kuwa sijafikia
kipimo cha mateso ya Baba zangu wa Imani.Lakini naamini nami yapo machozi ya
kufutwa ktk. siku Ile (japokuwa ni machache)
NAKAZA MWENDOOOO!!!!!!!!
MAPAPA(POPES)
Rumi ya kipagani iliwatesa Wakristo hadi
Karne ya 3. Kwenye Karne ya 4 aliongoka mtawala wa kirumi
aitwayeConstantine.Kuongoka kwake kulipelekea Kanisa kupumua kidogo mateso.
Kukoma Kwa mateso kulipelekea Kanisa kupokea waongofu wengi,Ila waongofu
nusunusu. Shetani akaitumia tena nafasi hii kuingiza uharibifu ndani ya kanisa.
Labda kabla sijaendelea
mbele nieleze kidogo juu ya kanisa la Roma na uongozi wa PAPA(POPE).
Jina Papa ,maana yake ni
"BABA" Lina asili ya kigiriki,"PAPA"
No comments: