MJI UDUMUO na Mwl.Nathanael Chaligha
Maana hapa hatuna MJI UDUMUO,Bali twautafuta ule ujao. Waebrania 13:14
Ndugu zangu katika Bwana,ule mji wetu ambao Bwana wetu Yesu alikwenda kutuandalia ,umeshakamilika tayari.Yohana14:2-3
Huu mji ni mzuri mno.Uzuri wake unapita maelezo yote ya lugha za kibinadamu.
Ni mji wenye misingi kumi na mbili(12);
Umezungushiwa kuta ndefu nzuri.Kuta hizi zina malango 12 ,ya kuiinglia huu mji. Milango mitatu,mitatu kila upande . Malango haya ni ya Lulu tupu.
Mji mzima umepambwa Kwa Vito vya thamani. Ulipambwa Kwa YASPI, YAKUTI SAMAWI,KALKEDONI,ZUMARIDI, SARDONIKI,AKIKI,KRISOLITHO,ZABARAJADI,YAKUTI MANJANO,KRISOPRASO,HIAKINTHO na AMETHISTO
Hivi ni vito vya thamani sana. Vinang'aa,uzuri wake hauna maelezo. Mungu amevitengeneza maalumu,Kwa ajili ya ujenzi wa mji huu. Havipatikani katika machimbo yoyote hapa duniani.
Njia zote za mji huu(streets)zimejengwa kwa dhahabu safi ing'aayo kama kioo.
Dhahabu hii siyo kama dhahabu ya dunia hii. Ile ni ya kipekee.Ina uzuri mno,uzuri wa kimungu.Haina mfano wake. Watakaoingia mji ule hawataisha kuishangaa.
Kando ya njia hizi za mji (streets) kuna mito ya maji inayotiririka kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu. Maji haya ni maangavu, yanang'aa kama almasi vile.
Kando ya mito hii,pande zote kuna miti mizuri itoayo matunda majira yote. Matunda yenyewe matamuuu. Kama ambavyo matunda yenyewe si ya kidunia,kadhalka utamu wake,huwezi kuulinganisha na utamu wowote wa kibinadamu. Mmh!!! Hapana ndugu zangu,NI UTAMU USIO KIFANI.!!!!!
Huu mji aliyeubuni na kuuchora(designer) ni Mungu mwenyewe. Na mjenzi(builder)ni yeye mwenyewe Mungu.Waebrania 11:10
Ikiwa wanadamu tu wanaweza kubuni na kujenga majumba ya kushangaza,Je,Mungu itakuwaje???
Nakuambia ndugu yangu, hakuna maelezo yatoshayo.
Mji huo urefu wake ni maili elfu moja na mia tano(1,500) Na mapana yake ni maili hizo hizo 1,500.Ni mji wa mraba,lakini cha kushangaza zaidi,urefu wa mji kwenda juu(maghorofa)ni maili hizo hizo 1,500. AJABU ILIYOJE??!!!!!!
Umbali wa Mbeya-Dsm ni wastani wa maili 800 hivi.Hivyo urefu wa mji huu ni kama kutoka Mbeya kwenda Dsm. na kurudi. Au urefu wake ni kama kutoka Lusaka(Zambia)hadi DSM. Waonaje mpendwa,ni mji mkubwa siyo???
Sasa na ijulikane wazi kuwa hayo maghorofa yatakuwa ndiyo makao yetu milele.Ufunuo 21:16.
Mji ule hauna maudhi na kero kama zilizopo kwenye miji yetu hii ya kidunia.
Kule hamna TRA wala DAWASCO,walaTANESCO hawana nafasi kule. Sikiliza,kule hakuna kudaiwa bill ya maji,umeme, kodi za majengo,wala Ada zà shule kule haziko.
Maisha ndani ya mji huo ,ni maisha ya raja iliyo timilifu,kwani Hamna magonjwa,wala misiba ya aina yoyote.Hakuna majanga, matetemeko,vita,mafuriko wala magomvi.Hakuna vikao vya suluhu kule.
Hakuna mahakama wala mapolisi.Kule hakuna kufunga milango kwani hamna vibaka,wezi wala majambazi. All,Shaban,All kaida, IS,wala Boko Haram hawajui kule.
Watakatifu watatembea kwenye viunga vya mji huu pasipo hofu yeyote.
Nuru Kali itatawala Jiji lote. Tutapishana na malaika kwenye viunga vya mji huu huku tukipeana heri milele.Watakatifu wa vizazi vyote toka Adamu,watalakiana huku wakiwa Wanajuana sana. Furaha yao itakuwa kuu sana,wala hakuna awaondeleaye.
Uzuri wa mji huu,na Ahadi ya Mungu Kwa watu wake,ahadi ya kuurithi mji huu, ndio uliowafanya watakatifu wote waishi Kwa Imani.
Abraham,hakuona Mali zake kuwa ni kitu cha kushikamana nacho. Kwa Imani akaishi ugenini kwenye hema, haikumsumbua kwani macho yake yaliuona mji huu,akautazamia Kwa shauku kuu.Waebrania 11:9-10
Shauku ya kuingia mji huu ndio uliowafanya watakatifu wavumilie mateso yote Kwa ajili ya Kristo. Walichinjwa,walichomwa moto,walidhihakiwa,walipigwa na kufungwa magerezani, walipigwa Kwa mawe na kukatwa Kwa misumeno,walikuwa hawana makao.Kazi yao ilikuwa kuzunguka-zunguka katika nyika na katika milima,mapango na katika mashimo ya nchi.
Kwa ajili ya Yesu,walikuwa maskini kuliko watu wote 1Wakorintho15:19
Watakatifu hawa Kwa wanadamu walikuwa kituko.(ni watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao.)Waebrania11:38
Hii ndiyo Imani ituwezeshayo kuingia mji ule.
Duniani hapa si petu,si mahali pa raha yetu. Sisi hapa tu wageni,tu wapitaji tu.
Baba zetu wote walikufa katika Imani hii,walikuwa hawajazipokea ahadi hizi,bali waliziona tokea mbali,wakazishangilia,na kukiri kwamba walikuwa wageni na wapitaji na wasafiri juu ya nchi.
Na watu wote hawa walishuhudiwa Kwa Imani yao. Waebrania11:13; 11:39
Yote katika yote,ni kukaa milele yote pamoja na Bwana huyu wa uzima,Yesu mwana wa Mungu. Atakuwa jua letu milele ndani ya mji huu. Tutakuwa naye Mungu wa miungu yote,Bwana wa Bwana wetu Yesu Kristo. 2Wakorintho5:1-10
JIJI HILI LINAITWA "THE BIG HOLY CITY OF JERUSALEM"
Ni Jiji zuri mno, limebuniwa na kujengwa na Mungu mwenyewe.
Liko tayari Kwa kuzinduliwa,limeshaisha kujengwa. Kinachosubiriwa ni walioandaliwa waingie.
Limeandaliwa Kwa waliojiandaa.
Je,mpendwa wangu umejiandaa?? Unangoja nini?? Huoni kuwa unachelewa???
Jiji lile ni takatifu,na hakuna kinyonge kitakachoingia. Jihoji na ujipime mwenyewe kama unatosha.
USIFANYE MZAHA YAPONYE MAISHA YAKO.
Kwa faida zaidi soma Ufunuo 21 na 22 kisha Waebrania 11
TUKUTANE NDANI YA " THE BIG HOLY CITY OF JERUSALEM"
No comments: