NEEMA YANGU YAKUTOSHA ,Na Mwl Nathanael Chaligha
NEEMA YANGU YAKUTOSHA
2WAKORINTHO 12:1-10(9)
Mungu anaitaka roho yako. Anaipenda hiyo ifike mbinguni aliko.Karama yako na vipawa vyako(ingawa vyatoka kwake)hana haja navyo sana.Angepewa kuchagua kati ya karama YAKO au roho yako ; angechagua roho yako. Nasema ; Mungu anaipenda roho yako zaidi ya karama zako.
Karama ya unabii; ualimu;;uponyaji;miujiza;kunena kwa lugha; uonaji; uhubiri na huduma zote za kichungaji; kitume; kikuhani; uaskofu; uzee; uinjilisti n.k. Haya yote kwa Mungu si kitu; bora ayakose hayo kutoka kwako kuliko kuikosa roho yako. Mara nyingi mambo hayo huleta majivuno tu. BIBLIA huyaita hayo "UJUZI" Ujuzi huleta majvuno bali upendo hujenga. 1Wakorintho 8;1(b)
Hii ndiyo sababu iliyompelekea Mungu kuruhusu Paulo kupata mwiba katika mwili wake. Mstari wa 7. Mafunuo yake na karama zake na huduma zake zingemletea tu kiburi; na majivuno juu ya wengine.(si unajua aliwazidi wote??)
Mwiba ule alijaribu kuung'oa ; ikashindikana. Alitembea nao maisha yake yote. Mungu alikataa kuung'oa; akasema;aaah!!!! NEEMA YANGU YAKUTOSHA( MST. 9)
NEEMA YA MUNGU YAKUTOSHA ndugu.!!!! Najua kuwa Mungu ameruhusu mwiba wa kukosa MTOTO katika ndoa yako. Pengine watoto unao lakini umaskini wa mfukoni umekusakama(huna pesa) Au ni magonjwa yasiyoogopa maombezi wala dawa. Au huenda mke wako au mume wako kwa tabia zake mbaya amekuwa mwiba kwako. Na labda mwiba wako ni kukataliwa na ndugu zako.
Sikiliza mpendwa; Acha kusikitika; acha kunung'unika. Mungu ameyaruhusu hayo kwa ajili ya kuipenda roho yako. Maadam NEEMA IOKOAYO Ijuu yako; sema hivi ;" NEEMA YA MUNGU YANITOSHA"
Najua unao udhaifu Fulani; ambao wewe unaujua zaidi ; basi ; jisifie huo kwa furaha nyingi; Upendezwe na udhaifu;na ufidhuli; misiba; kutengwa; kukataliwa; kunenwa vibaya; kusingiziwa; na shida zote kwa ajili ya Kristo" MAANA NIWAPO DHAIFU NDIPO NILIPO NA NGUVU.( MST.9; 10)

NEEMA YANGU YAKUTOSHA asema BWANA.
AMEEEEEN
AMEEEEEN
No comments: