AINA ZA WATU WENYE IMANI na Mwl.Dr Mwakisisile
Aina za watu wenye imani : basing on bishop Benson Idahosa. Aina ya kwanza undertakers , hawa ni watu wanaotumia muda wa makosa ya nyuma kuamua matendo yao ya leo. Wanaishi kwa dhambi za jana, wakijaribu kufanya jambo watakumbuka walivyokosea jana, mabaya ya jana watasimama. Kwenye biblia wanafanana na yule aliyeficha talanta yake. Hawa nao hawazai matunda, wameficha talanta zao. Kundi la pili ni Caretakers hawa hawakumbuki makosa ya nyuma bali utawaliwa na mazuri ya leo. Kila jambo watahimiza uangalifu, ni watu wenye taadhari wakiogopa kuwaudhi watu. Wanaangalia kila jambo maslahi yao binafsi bila kufikiria wengine. Hawafikiri wajiandae kwa ajili ya kesho bali raha yao ni leo. Kundi la 3 ambalo ndio nia yangu kuelezea ni Risktakers. Hawa hawatawaliwi na ya jana WAFILIPI 3:12-13 nasahau ya nyuma, nasahau walioshindwa, nasonga mbele, hawabebi hukumu za wanadamu 1wakorintho 4:3-4 , anasonga mbele bila kusikiliza kelele na hofu za waoga. Kielelezo chake ni Yesu na sio wanadamu. Nimalizie kwa kukutaka mpendwa usome 2wafalme 7 kuhusu wakoma wanne. Mstari wa 3 na 4 wanasema, tukikaa hapa tutakufa, tukienda kwenye kambi ya waaramu tutakufa au kupona, wakachagua kwenda mbele. Unahitaji kuchukua hatua, take risk , mashujaa wote wa imani walichukua risk. Hawakusimama kwa ajili ya walioshindwa, hawakusimama kwa ajili ya mafanikio, yote waliweka nyuma na kusonga mbele bila kujali nini kitawapata. Amina
No comments: